Maandalizi ya ‘wakubwa wa kesho’ ni hafifu
Na Asina Omari

Karne ya 21 imeitwa ni karne ya watoto. Kutokana na maana ya neno mtoto iliyotolewa na mkataba wa kimataifa wa haki za watoto tunaweza kusema kuna watoto milioni sita duniani. Yabidi tujiulize kuwa kama watoto ni nusu ya idadi ya watu duniani, je wanapata japo nusu ya huduma muhimu na rasilimali wanazohitajia?

Mkataba wa haki za watoto umeundwa juu ya misingi ya mahitaji muhimu ya watoto kwa kuzingatia kuwa utoto wa mtu unaathiri na kumuandaa mtu kuwa wa aina fulahi akiwa mtu mzima, pia kwa kuzingatia kuwa zipo tofauti za kimsingi kati ya watoto na watu wazima.
Moja ya kauli mbiu za mkataba huo ni watoto wa leo ndiyo wakubwa wa kesho. Hizo ni miongoni mwa jitihada za jumuiya ya kimataifa kujadili, kutizama na kuangalia mustakabali wa watoto katika dunia iliyo tawaliwa na wakubwa.

Mustakabali wa watoto ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Wakati wataalamu, washika dau na wakereketwa mbali mbali wanajadili masuala mbalambali kuhusu watoto na kutoa takwimu mbali mbali, inamlazimu mwanajamii yeyote kuangalia takwimu hizi katika muktadha wa jamii yetu.

Si zamani sana wataalamu katika fani husika (wa Tanzania) walikuwa wakijadili suala la watoto wa mitaani, magerezani na vituo vya kulelea watoto watukutu. Sababu zilizotolewa juu ya kuwepo kwa watoto wengi katika sehemu hizo zinachambuliwa hapa chini. Umaskini uliokithiri huwapelekea watoto kufanya uhalifu ili wapate kitu kidogo, pia huwafanya watoto washawishike kirahisi na kukubali kutumiwa na watu kufanya uhalifu. Umaskini hupelekea watoto aidha kwa hiari yao au kutokana na hali halisi ya nyumbani kujiunga na ajira(rasmi na zisizo rasmi) hali hii huwaweka kwenye mazingira mabaya ya uhalifu na kukosa maadili katika umri mdogo mno. Sote tunafahamu kwenye umaskini uliokithiri matumaini ya watoto kwenda shule ni karibu na mstari wa sifuri.

Familia imeelezwa kuwa ni mojawapo ya sababu ya kuwepo kwa watoto nje ya nyumbani mwao. Utafiti unaonesha watoto wengi waliopo jela, mitaani na katika vituo vya kulelea watoto watukutu wanatoka katika familia zenye matatizo, yaani zisizo madhubuti. Ukosefu wa maelewano kati ya baba na mama kunaweza kuathiri watoto kisaikolojia. Kutoelewana kwa watoto na walezi pia kunachangia hali hii.

Watoto wengi ni waathirika wa unyanyasaji wa nyumbani ambapo mtoto huweza kupigwa paspo sababu ya msingi na hata kutukanwa. Pia ni waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia (sexual harrasment) na haya hufanywa ndani ya familia na ndugu, jamaa au marafiki wa karibu. Hali hii inaweza kupelekea watoto kukimbia nyumbani, hasa anapokosa mtu wa kumfariji. Utafiti pia unaonesha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya watoto wa mitaani na uhalifu, vikiwemo vitendo vya wizi, kudokoa, kutumia mihadarati, ukahaba n.k. Malezi katika familia na jamii ndiyo yanayomtengeneza mtu awe wa aina fulani.

Kama mtoto hapati malezi muafaka kutoka kwa wazazi au walezi basi angalau malezi yapatikane kutoka kwa jamii na taasisi mbali mbali. Hii ni nadharia tu, sasa tujiulize katika hali halisi picha ya malezi ya watoto ikoje? Ni watoto wangapi leo hii wapo kwenye familia ambayo kila siku anamuona mama yake anapigwa na baba yake kwa vile tu kachelewa kumfungulia mlango alipo toka kilabuniau kumpelekea maji bafuni? Ni watoto wangapi wanaishi na mzazi mmoja, aidha kwa sababu mama na baba wameachana, eti kwa vile mke (mama) haelewani na wifi, shemeji au wakwe zake? Je katika jamii zetu hamna watoto ambao ni mayatima kwa kufiwa na wazazi wote wawili? Hamna huko mitaani kwetu mabinti waliokata tamaa na ufukara na kuona kuuza miili yao ndiyo nusra pekee waliyonayo? Mitaani mwetu hamna watoto wanao nyanyaswa na kudhalilishwa kijinsia na watu tunaowajua lakini tunaamua kufumbia macho eti tunaona aibu? Hatua inayofuata ni ya kujiuliza ni wapi tumekosea? Ni kwa nini katika kila kundi la vibaka, wezi, wazamiaji, wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya hawakosekani kundi hili?

Inakuwaje miongoni mwa machangudoa na mabaamedi ni vijana? Kwa nini watoto wengi wa mitaani na walio kwenye ajira zisizo rasmi ni wa walalahoi? Tufanye hesabu yanadharia kidogo. Chukulia kuna watoto kumi magerezani. Jawabu lako ndio asilimia ya watoto wetu walio magerezani. Jiulize ni asilimia ngapi ya wakubwa wa kesho ni wahalifu wa aina moja au nyingine, watoto wa mitaani hawapo gerezani?

Je wana elimu, wanakandamizwa kwa kutopewa fursa sawa n.k. Je ni nani tunamtegemea aje atuondoe katika hali hii? Wafadhili? Wapinzani? Nani ana uchungu na walala hoi hawa? Ukweli ni kwamba hali ni mbaya, kulaumu na kunyoosheana vidole hakusaidii, mikakati mipango na matendo ndiyo muokozi wetu. Tugundue na tulikubali tatizo kwani hiyo ni hatua moja mbele. Turudi kwenye misingi tuliyoiona haina maana tukaitupilia mbali. Tukichunguza sana tutagundua hamna anayetuonea na kutunyanyasa katika kuunda na kulea familia, sisi wenyewe ndio tumeiacha misingi aliyotuwekea Muumba wetu. Tumebadilisha misingi ya ndoa kutoka kwenye upendo, ucha mungu, tabia njema n.k. hadi katika yale tunayoyataka zaidi yaani mali, hadhi na uzuri.

Je mwanamke na mtoto leo hii wanapewa haki na hadhi walizopewa na Muumba wao au imebaki kuwa ni wimbo na mada katika mikutano, makongamano na mihadhara. Jamii yoyote ni lazima iwe na miundo( social structures or safety nets) je jamii yetu inayo miundo hii? Ni viongozi wangapi wanafahamu kuna mayatima, wajane na mafakiri wangapi katika maeneo yao? Kama kiongozi hajui takwimu muhimu (vital statistics) kama hizi ni nani anapaswa kufahamu? Je watoto na wanawake wanasehemu ya kukumbilia wakiwa na matatizo, ni nani anawafariji na kuwapa moyo wa kutaka kuiona kesho? Giza limeigubika jamii hasa wakubwa wa kesho.‘Juma’ ana miaka 10 anaomba omba mjini, mwaka 2011 atakuwa na hali gani kweli, tunamtegemea awe mkurugenzi wa shirika au hata karani? ‘Asma’ ana miaka 15 anajiuza kwa shilingi mia tu huko Manzese, hebu piga picha baada ya miaka 10 atakuwa wapi? Hawa ndiyo wakubwa wetu wa kesho!

Wakati wenzetu wanaanda